Chanzo Cha hospitali hii kilianza ukirejelea mnamo Tarehe 25 Octoba 1961. Chifu wa kabila la Ukinga mzee Kiluswa alitoa maombi maalumu kwa wamishenari wa Consolata akionesha uhitaji wa kituo Cha tiba katika eneo la Ukinga, wakazi wa eneo Hilo walikuwa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa rasilimali za afya na kiwango kikubwa cha kutisha cha vifo vya watoto wadogo.
Baada ya mfululizo wa mazungumzo na mamlaka zinazohusika, wizara ya afya na afisa wa kazi akathibitisha uanzishwaji wa hospitali katika kijiji cha Ikonda. Mnamo Tarehe 30 Novemba 1961 kwa kuanza na nyumba ya wamishenari, nyumba nne kwa ajili ya makazi ya ndugu wa wagonjwa na Pampu ya maji. Kati ya mwaka 1964 na 1968 Hospitali ilikuwa na uwezo wa vitanda 60, katika mwezi wa Februari mwaka 1968 kulikwa na ujio wa daktari wa kwanza mgeni kutoka Italia ambaye alionesha hatua muhimu, uzinduzi wa Hospitali hii ulijawa na Neema ya uwepo wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Tanzania mnamo Tarehe 7 Oktoba 1968.
Hatua mpya ya upanuzi ilianza katika mwaka 1974, kwa ujenzi wa majengo ya ziada ikiwemo Wodi ya watoto yenye vitanda 40, na ilikuwa Program Maalumu ya kupunguza vifo vya watoto wachanga, baadae maboresho yakafanyika kuhakikisha hali Bora ya usafi, nyongeza ya vyumba vya mashauriano ya wagonjwa wa nje na makazi kwa ajili madaktari wapya yalijengwa, sehemu muhimu ya rasilimali za Matibabu, Mashine za kutakasa, nazo pia zilinunuliwa.
Hospitali ikaendelea kukua na kufikia Uwezo wa kuwa na vitanda 180 ilipofika mwaka 1983. Kati ya mwaka 1996 na 2000 Hospitali ikawa kitovu Cha ushirikiano wa kimataifa kwa kuwaalika madaktari mbalimbali toka nje ikiwemo wapasuaji Toka Cuba, na wataalamu wa matibabu wa Uhispania, wakati wa kipindi hiki shirika la Uhispania Medicus Mundi, kwa ukarimu walitoa ufadhili kwa ajili ya utengenezwaji wa shule ya Kujifunzia yenye vifaa bora kwa ajili ya wataalamu wa Maabara, shule hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 75 kwa mwaka.
Mwaka 2000 ilikuwa ni alama ya mabadikiko makubwa kwa hospitali ambapo madaktari wageni wa mwisho waliondoka, katika hali hiyo hospitali ilikuwa ikiendeshwa na madaktari wenyeji. Mwaka 2004 hospitali ilianza program Maalumu kwa wagonjwa wa VVU na UKIMWI.Ilipofika mwaka mwaka 2007 kliniki hii ilikuwa imeshahudumia zaidi ya wagonjwa 15,000 kwa msaada maalumu toka kwa daktari wa Ujerumani Gerold Jagher, miaka 2002 Hadi 2008 ilishuhudiwa kuwa na viashiria vya ukuaji wa kipekee kwa kujengwa wodi mpya, vifaa vya kisasa vya matibabu kama vile mashine ya X- ray, vifaa vya maabara, maboresho yaliendelea kwa kuongeza miundo mbinu muhimu kama vile Matanki, spika za ndani na nje, na vyumba vya kufulia. Hospitali imesitawi kwa msingi wa ushirikiano wa kutembelea madaktari ma wauguzi, waliosimama kama taa ya matumaini na walijitoa kuhudumia jamii yao na zaidi